CHRONICX®: CHABA FT. NASH MC - USIPITE HAPA{PRODUCED BY DR.DAZ NALEDGE).

FOLLOW ME:

Instagram

Thursday, December 27, 2012

CHABA FT. NASH MC - USIPITE HAPA{PRODUCED BY DR.DAZ NALEDGE).

THIS TRACK IS FROM A-CITY EMCEE/RAPPER WHO GOES BY THE NAME OF CHABA REPRESENTING 009 CREW,THE TRACK GOES BY THE NAME PITA HIVI FEATURING EMCEE/RAPPER NASH MC FROM DAR-ES-SALAAM CITY AND ITS PRODUCED BY DR.DAZ NALEDGE FROM WATENGWA RECORDS:


Verse;1 (Nash Mc)


Nash mc eyoo sina bima wala sina mkorogo, ewura na vat,
Usiulize hapa, njoo barabarani kuanzia saa moja usiku utanipata,
Daladala chongo taa moja nawapaka,  Siti magunia kalia au acha,
Wee nani, Mc au rapper,  Maalim Nash ali nakuasa,
Usijaribu haya mambo mawili sio siri ntakukamata,
Kutaka kulewa au kumwiibia pasha, Ukishanasa, mtegoni nakupakata,
Mimi mwanajeshi lakini nyie wanajeshi wa marekani,
Mmeruhusiwa mnaingiliwa mpaka vitani, Wananiita Nash mc hardcore,
Mc chata bwana mc noma kona roba ya koo,
Frank zagarino John Rambo komandoo, Kova sio mwema kwenye patroo,
Saidi kubenea uchebe chata, niite papa John paul,  au Benedictoo,
Wasanii wabovu mnataka kuja nilipo, Njoeni taratibu msije mkaliwa jicho,
ah ah, jukwa lile silitaki wanavua mpaka boxer,
aaah, Napenda makalio lakini yenu yamechoka,

Chorus;

Nash mc, Daz Naledge, Chaba, usipite hapa utapigwa makofiii,
Nash mc, Daz Naledge, Chaba, usipite hapa utapigwa makofiii,
Wewee, utapigwa makofiii, wewee, hivi hauogopiii,
Wewee, utapigwa makofiii, wewee, embu pita hivi…….

Verse;2 (Chaba)

Umeniita Gabriel wa mistari kwa scenario,
Unapata sura funny kama scolio,  Kabla sijaku-crucify,
Nakuwashia ubani wa widi kutayarisha roho yako ku-fly,
Macho yanakutetema angali yako rai,
Inajua kinachofwata unaibusu hii game byebye,  Baridi ni ya kuganda,
Ila mwili joto kama upo njia panda,  Ya mercury na jua,
Yako rap laini kama ya waridi maua,
Imevaa kimini, highhills na hereni kwenye pua,
Ukinisoma, umesoma kitabu cha horror,
Chaba ni kimbunga chenye upepo wenye ugoro,
Unafilisika kuwaza, hii ni biashara ya kipaza,
Unatimbaje na mtaji wa rap kidogo,
Wakati hii vita baridi na wanajeshi mbogo,
Fimbo yangu ya maajabu kwa dada zako ni logo,
Wanaijua vizuri kama nyota njema ya mtaa,
Jogoo ninayetotolesha vifaranga wanaopaa,
Unataka jua hii, embu google my mixtape,
Pita hivi chalii, sisi ni madume ya rap,

Chorus;

Nash mc, Daz Naledge, Chaba, usipite hapa utapigwa makofiii,
Nash mc, Daz Naledge, Chaba, usipite hapa utapigwa makofiii,
Wewee, utapigwa makofiii, wewee, hivi hauogopiii,
Wewee, utapigwa makofiii, wewee, embu pita hivi…….
(LYRICS BY CHABBA 009)


No comments:

Post a Comment