CHRONICX®: RAPPA GAME NA 50 CENT KUMALIZIA MIKATABA YAO NA INTERSCOPE.

FOLLOW ME:

Instagram

Tuesday, October 2, 2012

RAPPA GAME NA 50 CENT KUMALIZIA MIKATABA YAO NA INTERSCOPE.

Marappa hawa wakongwe wawili yaani Game na 50 Cent ambae ni kiongozi wa kundi linalojulikana kama G-Unit wamesema kua wanatoa Album zao za mwisho chini ya interscope record kumalizia mikataba yao.Rappa 50Cent amesema kuwa album yake hiyo itaitwa Street king Immortal,itatoka mwezi novemba tarehe 13 mwaka huu(2012) na itakua na nyimbo kumi na Nne na Deluxe edition itakua na nyimbo kumina nane(Nyongeza ya nyimbo nne).Nyimbo inayotamba kwa sasa kwenye stesheni za redio ulimwenguni kutoka kwenye album hiyo ya 50 Cent unaitwa New day aliomshirikisha Mc/Rappa na Producer Andre young anaejulikana vema kama Dr.dre na Msanii wa kike wa RnB anaejulikana kama Alicia Keyz.Kwa Upande Mwingine,Album ya Rappa The Game itaitwa Jesus Piece ambayo itaachiwa mwezi huohuo pamoja na album ya 50 Cent.Nyimbo inayotamba kutoka kwenye albu hiyo ya The game kwa sasa kwenye stesheni za redio inajulikana kama Celebration aliyomshirikisha Rapper mkubwa wa kizazi kipya kutoka kundi la YMCMB, Lil Wayne na Rapper kutoka Taylor Gang anaeitwa Wiz khalifah pamoja na Msanii wa RnB anaejulikana vema kwa jina la Chris Brown.
50 cent
GAME

No comments:

Post a Comment